Genesis 36:19-40

19 aHawa ndio waliokuwa wana wa Esau (ndiye Edomu), na hawa ndio waliokuwa wakuu wao.

20 bHawa ndio walikuwa wana wa Seiri, Mhori, waliokuwa wakiishi katika nchi ile:

Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana,
21 cDishoni, Eseri na Dishani. Hawa ndio wana wa Seiri huko Edomu waliokuwa wakuu kwa Wahori.
22Wana wa Lotani walikuwa:
Hori na Homamu. Timna alikuwa dada yake Lotani.
23Wana wa Shobali walikuwa:
Alvani, Manahathi, Ebali, Shefo na Onamu.
24 dWana wa Sibeoni walikuwa:
Aiya na Ana. Huyu Ana ndiye aligundua chemchemi ya maji moto jangwani alipokuwa akichunga punda za Sibeoni baba yake.
25 eWatoto wa Ana walikuwa:
Dishoni na Oholibama binti wa Ana.
26Wana wa Dishoni walikuwa:
Hemdani, Eshbani, Ithrani na Kerani.
27Wana wa Eseri walikuwa:
Bilhani, Zaavani na Akani.
28Wana wa Dishani walikuwa:
Usi na Arani.
29 fHawa ndio waliokuwa wakuu wa Wahori:
Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana,
30 gDishoni, Eseri na Dishani. Hawa ndio walikuwa wakuu wa Wahori, kufuatana na makundi yao, katika nchi ya Seiri.

Watawala Wa Edomu

(1 Nyakati 1:43-54)

31 hWafuatao ni wafalme waliotawala Edomu kabla ya mfalme yeyote wa Israeli kutawala:

32Bela mwana wa Beori alikuwa mfalme wa Edomu. Mji wake uliitwa Dinhaba.
33 iBela alipofariki, Yobabu mwana wa Zera kutoka Bosra akawa mfalme baada yake.
34 jYobabu alipofariki, Hushamu kutoka nchi ya Watemani akawa mfalme baada yake.
35 kHushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi, aliyeshinda Midiani katika nchi ya Moabu, akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Avithi.
36Hadadi alipofariki, Samla kutoka Masreka akawa mfalme baada yake.
37 lSamla alipofariki, Shauli kutoka Rehobothi ngʼambo ya Mto Frati akawa mfalme baada yake.
38Shauli alipofariki, Baal-Hanani mwana wa Akbori akawa mfalme baada yake.
39Baal-Hanani mwana wa Akbori alipofariki, Hadadi akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Pau, na mkewe aliitwa Mehetabeli binti Matredi, binti Me-Zahabu.

40 mHawa ndio wakuu waliotokana na Esau, kwa majina, kufuatana na koo zao na nchi zao:

Timna, Alva, Yethethi,
Copyright information for SwhNEN